MO SALAH AIWEKA MISRI ROHO JUU
Misri ipo katika wasiwasi wa kumkosa nyota wake Mohamed Salah katika mechi iliyosalia ya kundi B baada ya mchezaji huyo kushindwa kuendelea na mchezo dhidi ya Ghana. Nahodha huyo wa Misri alilazimika kutolewa nje katika dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza kumpisha Mostafa Fathi baada ya kukaa chini yeye mwenyewe akionyesha ameshindwa kuendelea na mchezo kutokana na maumivu.
.
Hata hivyo, Misri bado haijaanika tatizo ambalo limemfanya mshambuliaji huyo kushindwa kuendelea na mchezo juzi lakini ripoti zinadai kuwa maumivu yaliyomfanya Salah asiendelee na mchezo ni ya misuli.
.
Na sasa Misri na klabu yake, Liverpool zinasubiria ripoti ya uchunguzi wa madaktari kufahamu tatizo alilopata na ukubwa wake ingawa wasiwasi umetanda kuwa huenda likamfanya akose mchezo uliobakia wa kundi lake dhidi ya vinara Cape Verde keshokutwa Jumatatu saa 5:00 usiku.
.
Mabingwa hao wa kihistoria wa Afcon ni lazima washinde dhidi ya Cape Verde ili wajihakikishie kutinga hatua ya 16 bora ya mashindano hayo baada ya kutoka sare katika mechi mbili za mwanzo dhidi ya Msumbiji na Ghana. Kocha wa Misri, Rui Vitoria alisema kuwa wana wasiwasi juu ya kilichotokea kwa Mohamed Salah ingawa alisema watajitahidi kuhakikisha hakiwatoi Mchezoni.
0 Comments