Achraf Hakimi mbele ya waandishi wa habari za michezo analitaja jina la Mbwana Samatta, anakwambia huyo ndiye mchezaji anayemjua zaidi na hakuna mwingine
Hakimi pamoja na kumjua Samatta lakini akaongezea kwamba, walaa hawamuhofii wao kama Morocco
Lakini hapa lipo jambo ndugu zangu, kitendo cha kumtaja Mbwana Samatta hiyo tu ni silaha tosha kwetu kuwabamiza hawa Morocco, naamini wataingia uwanjani akili yao yote itakuwa kwa POPA hiyo itatupa nafasi zaidi kuwatandika
Nyiee huyo Achraf Hakimi kumbukeni ni mchezaji mkubwa, mchezaji wa Dunia yaani siyo poa, Wajerumani, Wareno wote wanaijua shughuli yake huyo beki
Kucheza pale PSG tena Ligi kubwa Ulaya nchini Ufaransa siyo kitu kidogo, tunamuheshimu Hakimi lakini kesho kama Watanzania tuna jambo letu
Waliwahi kuja hapa hawa Wamorocco tukawapa chuma tatu, hii ipo kichwani kwao hadi leo kwaiyo kesho wataingia na tahadhari Kubwa wakiwa wanajua Tanzania siyo timu ya kinyonge
Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wetu ameshamaliza kazi ticket zote amezinunua ni sisi twendeni uwanjani
0 Comments