Hot Posts

6/recent/ticker-posts

SHAFFIH DAUDA ATOA HOSIA MZITO KWA SIMBA NA YANGA MSIKILIZENI


Ifike wakati Simba na Yanga wajitazame kama taasisi kubwa za kibiashara, wajitazame kama Wakongwe na watoke nje ya box kutumia mtaji wao wa Mashabiki na Wanachama, hakuna timu kubwa duniani ambazo ni Wapinzani na hawajatumia upinzani kibiashara. 

Ukienda derby ya Soweto, Afrika Kusini wana Black lebel Cup ambapo Kaizer Chiefs na Pirates wanapiga mzigo wa kutosha sana, hapa kwetu tulikuwa na Mtani Jembe kabla ya mmoja kuachia unyoya, inafikirisha sana. 

Ukienda Spain, Real Madrid na Barcelona hawa kwanza wana makubaliano ya kutoingiliana kwenye sajili lakini pia ndio waliopigania sana haki za maudhui yao kutouzwa kwa Mchina kwa bei ya madafu, huku kwetu wanazungukana kila mmoja anapita njia yake. 

Ukienda Milan wana mbungi ya Madonina kati ya Inter na AC Milan, hawa baada ya muda mrefu kutumia uwanja wa Manispaa wameamua kujenga uwanja wao na serikali imewapa eneo kutokana na ukubwa wao, wameingia ubia na wanafyatua kitu cha maana, huku kwetu kila mmoja anaimba wimbo wake. 

Simba na Yanga ondokeni kwenye mitazamo ya miaka ya 80 wakati sukari ni shilling 100 na maduka ya Ujamaa, njooni kwenye dunia ya sasa, mna mtaji mkubwa sana ambao mmeshindwa kuutumia hata nusu mpaka sasa, miti ni mingi ila hakuna wajenzi, inafikirisha sana mpaka sasa. 

Mimi nawaona mnaishi kwenye dunia yenu ya kufikirika ya kubishania idadi ya makombe, wafuasi mitandaoni lakini sehemu sahihi bado hamjaigusa, hii inaanzia kwa Viongozi bado hamjagusa sehemu sahihi, hit the spot and the rest will be history. 

DIGALA IS OUT!

 

Post a Comment

0 Comments