Simba kabla ya kushuka uwanjani kuikabili Al Ahly ya Misri kwenye mchezo huo, tayari Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeshaipa mkwanja wa maana usiopungua Dola 400,000 (Sh 1 bilioni).
Simba imelazimika kuchukua fedha hizo baada ya CAF kupunguza kutoka viwango vya awali na ilikuwa kila timu inayoshiriki katika hatua hiyo ya robo fainali ilikuwa ivune Dola 1 milioni (zaidi ya Sh 2.5 bilioni) kabla ya kupunguzwa na kuwa hizi Sh 1 bilioni kwa mujibu wa viongozi wa Simba.
Mabosi wa Simba wamepanga kutumia fedha hizo kiasi kikubwa kwa wachezaji wao, lakini hesabu zao wakitaka timu yao iwapeleke hatua ya nusu fainali ambayo watavizia kiasi cha 2.2 bilioni endapo watatinga hatua hiyo kwa kuwaondoa Ahly.
Awali bingwa wa michuano hiyo ilikuwa anazoa Dola 4 milioni (zaidi ya Sh 10 bilioni), huku wa pili atazoa Dola 3 milioni (zaidi ya Sh 7.5 bilioni) wakati timu itakayiotinga nusu fainali itakomba Dola 1.7 milioni (zaidi ya Sh 4.3 bilioni), hata hivyo kuna mabadiliko yamefanyika kimyakimya.
Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Salim Try Again amesema; “Ni kweli kuna hilo suala la hizo fedha watu wafahamu hivyo viwango kwanza vimebadilishwa, nadhani CAF watatangaza baadaye, lakini sisi Simba tunalijua hilo.”
Mbali na fedha za African Football League, Simba imejihakikishia pia kuvuna kiasi cha Dola 700,000 (karibu Sh 1.8 bilioni) kwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kama ilivyo pia kwa Yanga iliyofuzu hatua hiyo baada ya miaka 25 iliyopita.
0 Comments