Hot Posts

6/recent/ticker-posts

TAIFA STARS KUTWAA UBINGWA WA AFRICA HIVI KARIBUNI


🗣️Nina Imani kubwa uongozi wa shirikisho la soka Tanzania chini Rais Wallace karia katika mipango ya kuhakikisha soka la Tanzania likuwa kwa kasi na kuwa shindani dhidi ya mataifa mengine katika soka

🗣️Chini ya Rais Wallace Karia tumepata nafasi ya kwenda kwenye fainali za Afcon kwa mara ya pili, 2019 nchini Misri na fainali zijazo nchini Ivory coast 🇨🇮,Hii inamaana kubwa sana kwenye soka la Tanzania 🇹🇿, Uongozi unajitaidi sana kutengeneza mipango ya kutawala soka la Africa ingawa baadhi ya wadau wengi wanapinga billa kuwa na hoja za msingi

🗣️Benchi la ufundi la Taifa stars chini ya kocha Edel Amrouche na Hemed Morocco na wasaidizi wake, Ujio wake ndani Taifa Stars hakuwa na mbwembwe na kupelekea wadau wengi kutomwamini, Lakini ni kocha anayetambua soka la Tanzania linahitaji nini, Mabadiliko yake kwenye kikosi yamekuwa na faida kubwa, Maboresho ya kimbinu na kuboresha viwango vya wachezaji wetu,Kuamini nguvu vijana na kufanya utafiti pia kwa wachezaji wanatoka nje ya ligi yetu



 

Post a Comment

0 Comments