Mashabiki wa Simba ni wajibu wao kuwafanya CAF wasijutie kuamua kuileta Tanzania mechi ya ufunguzi wa mashindano ya African Football League [Simba V/s Al Ahly].
Pamoja na mambo mengine, CAF wanatarajia kuona mechi inapata watu wa kutosha uwanjani. Kwa hiyo uwanja ukijaa, itawavutia CAF kuona namna ambavyo mechi ya kwanza ya uzinduzi/ufunguzi wa mashindano haya imepokelewa kwa ukubwa.
Kwa hiyo mashabiki wa Simba wanapaswa kutoiangusha klabu yao lakini pia hawaifanyi CAF kuona ilifanya uamuzi makosa kupeleka mechi ya ufunguzi sehemu ambayo haikustahili.
Mechi hii ya Simba V/s Al Ahly inaweza kuwa kipimo pia kwa mashabiki kuwa wana utayari kwa kiasi gani kupokea mashindano makubwa kuelekea AFCON 2023, ni muhimu kuonesha kuwa tulikuwa tunahitaji kuwa sehemu ya mashindano makubwa ya aina hiyo.
Ni muhimu kwa mashabiki wa Simba na mashabiki wa soka kwa ujumla kwenda uwanjani siku ya Oktoba 20, 2023 kuujaza uwanja kuipa thamani mechi na mashindano yenyewe.

0 Comments