Mama mzazi wa mshambuliaji Kylian Mbappe amekiri kulumbana na mwanaye baada ya kuhitaji alipwe asilimia 50 ya kile anachovuna mchezaji huyo ndani ya uwanja.
.
Mama wa mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain, mrembo, Fayza Lamari ndiye wakala wake. Lakini, mama huyo aliyekuwa mchezaji wa mpira wa mikono, 49, alimkasirisha mwanaye baada ya kumwambia anahitaji nusu ya Pauni 46 milioni ambazo analipwa mshambuliaji huyo huko PSG.
.
Fayza alisema namna alivyojibiwa na Mbappe baada ya kutaka alipwe nusu ya mapato yake, alisema alichojibiwa na mwanaye: “Siwezi kukupa hiyo asilimia 50. Una tatizo gani? Mimi ndiye nafunga mabao, wewe unataka nusu ya mapato kwanini?”
.
Mbappe mkataba wake huko PSG utafika tamati mwishoni mwa msimu huu na amekuwa akihusishwa na mpango wa kwenda kujiunga na Real Madrid. Hata hivyo, ripoti za hivi karibuni zinadai PSG imeweka ofa ya kumlipa Mbappe Pauni 86 milioni kwa mwaka ili kubaki na huduma ya mchezaji huyo kwenye kikosi chao.
0 Comments