PESA HIYOOOOO .!
Unalipa Pauni Milioni 105 kwa mchezaji kama huyu , sio wengine mnalipa 100 hovyo hovyo tu .!
Size ya pitch ya uwanja wa Luton ni changamoto aisee hasa kwa passing game
✍🏻Kwa kiasi kikubwa hasa kipindi cha kwanza Gaby Jesus alikuwa anasaidia sana kwa Arsenal kusogea juu kwa
1: Kushuka chini , kupokea mpira na kusogea nao juu ( carries )
2: Kushambulia space baina ya outside CBs wa Luton na wingbacks wao
✍🏻Luton wanastahili pongezi kwa mpango wao : walitumia faida ya udogo wa pitch kwa kubana zaidi space na kutumia counter attacks plus mipira iliyokufa kupata chochote kitu .
✍🏻Kipindi cha pili ni kama vile ilikuwa nani atafunga magoli mengi zaidi ya mwenzake , mmoja anatumia ufundi wa kuweka mali chini ( Arsenal ) mwingine anatumia ufundi wa mipira mirefu na iliyokufa ( Luton ) : mwisho Arsenal wakawapa Luton ladha ya dawa yao wenyewe . Heartbreaking
NOTE
1: Yule Fullback wa kushoto wa Luton : Doughty ana mwaga maji huyo
2: Ross Barkley kama alikamia vile , kaubonda
3: Kai Havertz anakuja bhana , kajipata tayari
4: Bukayo Saka ni hatari , anafanya vitu kwa level ya juu sana
5: Gaby Jesus kuna muda anakuwa Yes kuna muda No
6: David Raya 🤔 nafikiri Ramsdale atakuwa na matumaini nafasi yake bado ipo
7: DECLAN RICE , DECLAN UBWABWA ... PESA .! What a player . Tangu atue Arsenal sikumbuki mechi gani alicheza vibaya . Arsenal waongeze zingine £20M kwa West Ham
8; Kafungwa Luton lakini wanachukia wengine . 😀
FT: Luton 3-4 Arsenal
0 Comments