Hot Posts

6/recent/ticker-posts

SIMBA SC WAFUZU KIBINGWA KWENDA ROBO FAINALI KWA USHINDI WA GOLI SITA


SIMBA SPORTS CLUB, Muungwana mmoja alisema “Simba wajifunze kwa Yanga” akasahau mstari wa Ibrahim Mussa wa Tanga, Roma Mkatoliki wa Tongwe Records aliwahi kuchana “Imaam akizini nje ya ndoa, usiukimbie msikiti” na “Padre akilala na Sista haibadilishi Ukatoliki” hizi ni hatua kubwa kwa ajili ya wakubwa, lights on! Sounds on! Big Dawgs have signed in style. 

The Robo Fainali Challenge is accepted! Mnyama anafanya kwa mara ya tano, sio stori kubwa sana kwake ni kama Binadamu kula Samaki sio stori kama ambavyo Samaki kula Binadamu ndio stori, Mnyama kwenye hatua zake za siku zote kama Msechu na nyimbo za maombolezo, kama mitaa ya Riverside na Utelezi, hello did you miss them? 

Dust off your Sandaland Kits! Kwakuwa msimu bado unaendelea kwa Mnyama, wakati Taifa linamlilia Rais wa awamu ya pili Simba Sports wakafanya ukatili mizinga 21 ya JWTZ na mizinga sita ya Simba, siku bora ya kumuaga Half Back kwenye dunia ya soka la sayansi, Che Malone the Football Guevara, Henock Inonga na shule ya Mabeki muite Skonga! From Manga Pwani to Mashariki mwa Pwani, Karibu kwa show za Babacar Sarr the Football Kuhani. 

Fabrice Ngoma from Kongo with Love, Football by Passion! Galaxy na script ya Makhirikhiri ukazimwa mziki, sauti ikabadilika ni wasaa wa kucheza boringo, beat imevuja damu na imechezwa bila huruma! Walileta mitikasi they just had to line up na kuicheza ndomboro ya Kimang’ati! Unamtazama The Real Number 6 kabla ya Amapiano Boy, kutoka Airport mpaka kwa Mkapa, msimu wa kwanza na robo fainali! Gari haitaki Dalali ni push to start. 

Mr Ben Twitted, Mama Kanisa anaadhimisha Dominika ya 3 ya Kwaresima Mwaka B wa Kanisa, Himizo kubwa katika kipindi hiki ni toba na wongofu wa moyo na muunganiko na Mungu kwa njia ya sala! Thank you Catholics na sisi tunasema Mtoto Galaxy hatukumnyima mapigo, Waraka wa Kocha Benchika kwa Wagalatia, you all put your hands up when Reds are up for the game, we mean business. 

We are witnessing Football heritage Live and direct! Million 30 hazihitaji ukaguzi wa CAG! Just to remind you, Njuka kwa mara ya kwanza na Kidato cha tano kwa mara ya tano! 

VISIT MOROGORO🇹🇿

 

Post a Comment

0 Comments