Hot Posts

6/recent/ticker-posts

ENZI HIZO SIMBA ZA DO OR DIE, NDANI YA ESTADIO BENJAMIN MKAPA.

 


Imeandikwa Na @jr_xavihernandez.


Ni saa moja kamili usiku, Kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa hakuna  tena kiti kilichokuwa wazi ni full house, Usiku ule uwanja wa Benjamin Mkapa uligeuka kuwa Signal Iduna Park ambao ni uwanja wa Borussia Dortmund.


Usiku ule Simba wakiwa na kauli mbiu yao ya Do or Die, Wakaandika historia ya kutopoteza mchezo hata mmoja wa nyumbani kwenye hatua ya makundi ya Klabu bingwa afrika.


Ni usiku ambao 4:2:3:1 ya mwalimu Florente Ibenge inakwenda kumezwa na 4:3:3 ya mwalimu Patrick Aussems, Ni mechi ya machozi,jasho na damu.


Katikati ya dimba la As Vita wana mwanaume mmoja hivi jezi yake namba 8 mgongoni miguu yake ni ya Italy na maamuzi ya Brazil, Aliitwa Fabrice Ngoma, Fundi sana.


Mapema Kazadi Kasengu anawatanguliza As Vita, Presha inaongezeka nje ya uwanja, Lakini wanaume 11 wa Simba hawakubali kabla ya mapumziko tu, Mohamed Hussein anafanya ubao usomeke 1-1.


Simba wanaamua kuvaa uhalisia wao, Alikufa Al Ahly akiwa na kikosi chenye thamani zaidi ya  Bilion 80 Ni kina nani hao As Vita? Mpira unapigwa mwingi kwa kushambuliana basi Benjamin Mkapa inapata ladha kamili ya mchezo.


Baadae maarifa ya Fabrice Ngoma yanashidwa kufanya kazi mbele ya Mzamiru Yassin, Akili ya Nelson Munganga ikawa ya kufikirika mbele ya James Kotei. Ni Do or Die.


Mungu aendelee kuubariki ubongo ule wa Patrick Aussems na zile sub zake, Okwi, Mzamiru na Kotei nendeni nje, Niyonzima,Dilunga na Rashid Juma nendeni ndani.


Unawezaje kumtoa kiungo mkabaji kwa dakika zenye mashambulizi kama zile? Aussems hakujali. Niyonzima na Chama Double 8, Rashid Juma anatembea sana kule kushoto.


Haruna Niyonzima aliingia na sura ya Luca Modric, Aliutawanya mpira atakavyo alichukua timu kutoka chini na kuisogeza juu mpira ulikuwa unamtii, As Vita usiku ule hawakuwa na dawa kwa mtoto wa Gisenyi.


Basi Zana Coulibaly na Bocco wanatembea sana kulia, Bocco anapiga pasi moja hatari, Niyonzima anauacha mpira na unamkuta Mwamba wa Lusaka.


Chama akafanya kama Andres Iniesta kwenye fainali ya Kombe La Dunia pale Afrika ya kusini. Kilichobaki ni historia tu. Mnyama huyo Robo fainali ya CAF, Siku zimetukimbia sana.

Post a Comment

0 Comments