Hot Posts

6/recent/ticker-posts

KWANINI MSHAMBULIAJI WA NIGERIA NA TIMU YA NAPOLI Victor Osimhen HAVUI MASK UWANJANI?

 


Kumekuwa na Maswali Mengi kwa wadau mbali mbali wa soka wakiuliza ni kwanini Victor Osimhen 🇳🇬 bado anavaa Mask hadi leo?


Je haponi? Na Je, atavaa hadi lini?


JUA KWAMBA: Osimhen alipata jeraha baya usoni, katika mgongano wa vichwa na beki Milan Skriniar wakati wa mchezo wa Serie A kati ya Napoli na Inter Milan mwezi Novemba 21, 2021.


Aliporejea uwanjani kutoka kwenye jeraha lake akaanza kuvaa Mask usoni ambayo kwasasa imekuwa kawaida kwake.


Akizungumza katika mahojiano na Brilla FM, Osimhen ambaye kwa sasa yuko kwenye majukumu ya kitaifa na Super Eagles kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, nchini Ivory Coast, alisema ni hatari kwake kucheza bila Mask.


"Ni hatari kwangu kama nitacheza bila hii Mask, Lazima nivae Mask katika maisha yangu ya soka kwa sababu nina screws kwenye taya na uso wangu. Bado ninazo hadi sasa,”


" Mechi ya hivi karibuni dhidi ya Cagliari nilipofunga goli kwa mpira wa kichwa kulikuwa na damu ambayo ilikuwa imechora muonekano wa mask yangu" 


 "Kwa hivyo ni hatari kwangu kama nitacheza bila kutumia Mask, iko hivyo."


Imeelezwa kuwa Osimhen ana screws 18 za chuma na plaques sita zimewekwa ili kuimarisha sura yake ya usoni kutokana na jeraha hilo kubwa alilolipata.


#sokaonlineupdates

Post a Comment

0 Comments