Yannick Litombo Bangala is One of the Best Player 🧠✅ Kipindi yupo Young Africans chini ya Mohamed Nabi alitumika kama Kiungo Mkabaji lakini pia Mlinzi wa kati mara kadhaa, Timu ilionekana kuwa imara sana kwenye eneo la kiungo mpaka eneo la ulinzi pale alipocheza kama Kiungo Mkabaji
Eneo la kiungo alipocheza alitekeleza jukumu muhimu la la msingi la kuzuia walinzi wake wa kati kutofikiwa sana na Timu pinzani lakini pia kupunguza makosa mengi ambayo yalikuwa yanafanywa na Viungo wake wa juu(Attacking Midfielders)
Majeraha, kushuka kiwango, mabadiliko ya muundo wa timu n ubora wa wachezaji wengine katika maeneo aliyokuwa anacheza ukapelekea kupoteza uhakika wa kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Young Africans chini ya Mohamed Nabi
Kilichofuata baada ya hapo ni YANICK BANGALA kuhitaji changamoto mpya lengo ni kwende kupata walau nafasi ya kucheza katika klabu nyingine nje ya Young Africans, Kila kitu kikaenda vizuri na Mchezaji akafanikiwa kujiunga kwa matajiri wa Dar Es Salaam, AZAM FC
Ndani ya Azam FC amefika muda wa kuanza msimu mpya wa mashindano ukiwa karibu wakati ambao pia yeye ana majeraja hali iliyofanya mpaka sasa anapata wakati mgumu pia kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha Azam FC chini ya Youssouf Dabo na Bruno Ferry
Quality ile ya YANICK BANGALA kama Azam FC wataipata tena kutoka kwenye miguu yake basi naona kuna kitu kikubwa sana kitaongezeka hasa kwenye muundo mzima wa uzuiaji wa Timu yao, Mapinduzi Cup ya Msimu huu kama ataitumia vizuri basi tunaweza kupata ubora wake tuliouzoea.
Welcome Back YANICK LITOMBO BANGALA 🧠👊
@officialevodiusoscar_
0 Comments