
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephanie Aziz KI yuko kwenye kiwango bora msimu huu na sasa ubora huo umemchongea kocha wa Timu ya Taifa ya Burkinafaso, Hubert Velud.
Kocha Velud amejikuta kwenye presha kubwa juzi wakati akitangaza kikosi cha taifa akikaliwa kooni juu ya matumizi ya Aziz KI anapojiunga na timu ya taifa hilo.
Iko hivi mashabiki wa Burkinafaso huwambii kitu kuhusu Aziz KI hasa baada ya staa huyo kuchagua kulitumikia taifa hilo badala ya Ivory Coast ambako familia yake inakaa.
Kocha Velud amesema kuwa “Kazi yetu kama makocha ni presha wakati wote, najua kiu ya mashabiki wanatamani kuona wachezaji wao wote sio tu KI (Aziz) wanacheza kwa ubora timu ya taifa kama ambavyo wanajituma klabuni kwao,” alisema Velud ambaye aliwahi kukaribia kufanya kazi Simba na Yanga katika nyakati tofauti.
“Tangu nianze kazi hapa nimekuwa kwenye mawasiliano bora na makocha wa Yanga Nasreddine (Nabi) na sasa nataka kuzungumza na huyu wa sasa (Miguel Gamondi) lengo ni kutaka kuona anaendelea kuwa bora, ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa na sasa yuko sawasawa zaidi.”
0 Comments