
Nyuma ya kipigo kikali cha 5-1 kutoka kwa Yanga kulikuwa na kelele tatu kwa mpigo ambapo iliyokuwa na nguvu zaidi ni MFUMO WA UTAWALA ya pili ikaja KOCHA MKUU na ya tatu ikaja WACHEZAJI.
Huku na huku Kocha akatupiwa virago vyake lakini haikuweza kuzima kelele za Mashabiki na Wanachama kuwa ni wasaa wa VIONGOZI nao kuachia ngazi na kupisha maono mapya, kelele zikaendelea kila upande kwakuwa ukweli wa kupanda ngazi hatimae umefika.
Ghafla sana ikaja stori isiyofahamika wapi imetoka, stori hiyo ilishusha tuhuma nzito kuwa WACHEZAJI KADHAA WAMEUZA MECHI, wengine wakaenda mbali kabisa na kuwaita Wachezaji hao kuwa ni MADUKA, hizi ni tuhuma nzito sana kwa Wachezaji na klabu, lakini kwa ufahamu wangu ni SPINNING ile ile ya kuhamisha goli kwenye hoja ngumu na nzito ya MFUMO WA UTAWALA.
Lakini ukweli uliokuwa unakuja taratibu tena kwa kupanda ngazi unafahamu kuhusu propaganda za maksudi kuwatoa watu kwenye hoja muhimu, mara unasikia Mwenyekiti kaambiwa ajiuzulu, mara Ahmed amekalia kuti kavu yote ni KUHAMISHA GOLI kuwa Simba ina shida sehemu.
Nini kifanyike kwasasa?
1- Kila Mwanasimba akapitie Katiba ya Klabu yake, aelewe Mfumo wa Utawala ulivyo! Kwa kifupi sana Wajumbe wa Bodi waliochaguliwa na Wanachama pamoja na Chairman Mangungu kwenye mfumo wa klabu hawa ni CEREMONIAL LEADERS hawana nguvu yoyote, hivyo kimsingi upande wetu umezidiwa.
Mwenyekiti wa Simba hasimamii Mradi wowote na sio Mkuu wa Oparesheni ndani ya klabu, klabu ipo kwa CEO na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, hapa kwanza tujue ili tufahamu Katiba tuliyopita ina matobo kiasi gani.
2- Klabu itaendelea kuganda hapo mpaka pale itakapoweza kuandikisha Wanachama wapya ambao 90% watakuwa Vijana na maono mapya, wawe na sifa za kugombea ili wakaweke hayo mawazo, nje na hapo Wanachama wachache waliopo ambao waliingia muda wataleta mabadiliko?
MUHIMU, Mchakato wa mabadiliko ukamilike! Klabu iandikishe Wanachama wapya hapo itakuwa mwanzo wa zama mpya, nje na hapo tuendelee kuvumilia na huo ndio ukweli mchungu.
GOLI HALIPASWI KUHAMISHWA, GOLI LIPO PALE PALE KWA MFUMO WA UTAWALA.
VISIT MOROGORO🇹🇿
0 Comments