Hot Posts

6/recent/ticker-posts

SABABU MILLION KWANINI VIONGOZI WALAUMIWE

Uploading: 307846 of 307846 bytes uploaded.


KIKOSI, Simba hii sehemu kubwa ya Wachezaji 70% ni wale wa misimu sita nyuma ambao ndio sehemu kubwa ya waliobeba Premier mara nne, FA Cup na Ngao huku wakitamba Afrika, kimpira washafika vilele vingi hawatokuwa na njaa ile ile ya misimu minne nyuma! Je kuna succession plan ambayo Viongozi wameiandaa? Njia ipi mpya?


UBORA WA KIKOSI, nimeona hoja kuwa Wachezaji hawajitumi lakini kujituma huendana na changamoto mpya ya ubora wa wachezaji! Kwa kifupi Mohamed Hussein awe na mtu wa kariba yake kwenye bench, Chama Clatous, Saido Ntibazonkiza, Fabrice Ngoma, Shomari Kapombe, Kibu na wengine wengi hawana mbadala wa kufanana nao kwenye bench. 


Suala sio kulipwa mshahara mkubwa suala ni kutumikishwa uwanjani na kuhofia namba! Nenda Yanga una Kibabage na Lomalisa, una Kibwana na Yao Yao, una Nondo, Bacca na Job kisha katikatia ndipo pamejaa haswa! Hawa lazima kujituma ukilala umeisha! Bado wastani wa umri, kwenye intensity timu itamudu? Rejea game zote za mwendo mpaka ya Mtibwa.


SCOUTING, Viongozi wamemleta Mtalaam wa Scouting wakati usajili unaendelea mtanikumbusha vyema! Scout anaripoti kwa Mkurugenzi wa Ufundi, je ni nani huyo pale Simba yupo? Hayupo! Technically anaripoti kwa Viongozi, sasa kama wao wanahusika kwenye usajili mbona timu ikifeli kafukuzwa Kocha pekee? 


MABADILIKO YA KIMFUMO, hapa ni sehemu muhimu hawa Viongozi waliopo madarakani wamefanya jitihada gani timu kukamilisha mabadiliko? Timu ina miaka sasa haichukui Wanachama wapya, Wanachama ni sehemu muhimu ya mabadiliko ya klabu, unadhani damu changa zikiingia kwenye mikutano watahitaji hii katiba? Jibu ni HAPANA. 


USASA, Gym yetu ipo wapi? Vifaa vipoje? Naishia hapo. 


Wanachama wapya wataleta fedha kwa klabu na mawazo mengine mapya, klabu itasogea kwa kiasi kikubwa! Kila siku mnaenda JNICC wanachama makadirio 2,000 tu vision na mission inajadiliwa na wale wale, Mwenyekiti hana nguvu hawajali hata. 


MWISHO, klabu kubwa zote duniani ikitokea kadhia kama hizi Viongozi huomba radhi nadhani mjitokeze muombe radhi na sio baadhi ya Mashabiki maarufu kuja kuwasemea, kisha yabebeni yale ya muhimu mnayoshauriwa na klabu isonge! Viongozi mna 70% ya lawama zote.

Post a Comment

0 Comments