
SIMBA imeanza msako wa kutafuta kocha kwa kasi wa kumrithi aliyekuwa Kocha Mkuu wa Roberto Oliveira ‘Robertinho.’ Na habari zinashtua mtaa wa pili, yaani kule Jangwani ni kwamba mabosi wa timu hiyo fasta wamemrukia aliyekuwa Kocha wa Mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga, Nasreddine Nabi.
Nabi ameijulisha familia yake juu ya simu hiyo iliyomshtua akiwaambia amefanya mazungumzo ya awali na wekundu hao ambao waliwahi kufanya makosa ya kumtaka kisha kumuacha.
Nabi alitakiwa na Simba awali alipokuwa na Al Merrikh ya Sudan kabla ya kumpotezea kutokana na kutimuliwa na timu hiyo.
Mabosi wa Simba wanaamini kwa hali iliyopo kwenye timu, yeye ndiye kocha mwafaka kuirudisha kwenye ramani ya kutamba kama ambavyo alivyofanya kwa watani wao Yanga ambao bado wameendelea kuwa juu licha ya Mtunisia kuondoka.
“Ni kweli Simba wamemfuata baba, lakini sitaki kuliongelea hilo kwa undani kwa kuwa kwa sasa kocha yupo kwenye mkataba na FAR Rabat ni vyema hili likaheshimika kwanza,” alisema Hedi Nabia ambaye ni mtoto wa kocha huyo
Via mwanaspoti
0 Comments