HAYO NDIO MAMBO SASA
Zipo taarifa za klabu ya Simba SC kuanza kufanya mazungumzo na kocha Florent Ibengé ambaye kwa sasa anaifundisha Al-Hilal Club ya Sudan
Hizi ndio habari ambazo mashabiki na Wanachama hupenda kusikia siyo vinginevyo
Ukipoteza unakubali na ukianguka unakubali pia, ukweli ni kwamba Simba SC ilishuka lakini uongozi ulikuwa umejifichia kwenye matokeo ya kumfunga Yanga SC mabao yale mawili na ile Fainali ya Ngao ya Jamii
Tatizo lipo hapa ukianza kuandika kuhusu mapungufu yaliyopo watakuvika kuwa wewe ni Chawa au umetumwa ili uje kuisema vibaya timu yao, lakini bila ya kukosolewa huwezi kuona mapungufu yako
Simba SC ikifanikiwa kumchukua Kocha Ibenge bila shaka wataanza kuingia katika moja ya malengo Kutokana na ukubwa wa huyu Kocha pamoja na CV zake
Mwaka 2014 - 2019 aliwahi kuifundisha timu ya Taifa ya DR CONGO huku akiwa Mwalimu wa AS VITAL CLUB mpaka 2021
Florent Ibengé pia aliwahi kuifundisha timu ya Shanghai Shenhue ya China mwaka 2012, kwaiyo utaona namna gani alivyoweza kupita pita katika nchi mbalimbali ambazo ziliweza kumpa ukomavu
Usisahau mwaka 2021 - 2022 pale RS Berkane na sasa yupo zake Al-Hilal Club ya Sudan
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakuregenzi ya Simba SC, Abdallah Try Again' Muhene akianza kuzungumza ukubwa wa Simba anapaswa kuanzia huku Kwa kuijenga timu vilivyo ili alete Ushindani wa kweli na siyo ile ya kutuambia kauli za Rais wa FIFA kwamba, Simba SC inacheza mpira mzuri kuizidi Mamelod Sundown, Wydad Casablanca
Kwa kauli hizo waulize wana Simba wenyewe je wanakubaliana kwamba, Simba inavizidi hivyo vilabu kwa ubora kama alivyosema?
Karibu kwa kujibu hilo swali hapa, lakini kuingia kwenye mazungumzo na Kocha Florent Ibengé ni habari njema zaidi kuliko mambo mengine
0 Comments