HILI LILIKUWA LINAKUJA
✍️Siku kama hii ilikuwa inakuja kwa Simba SC, ni basi tu hatukujua itakuja kutokea dhidi ya timu gani ila ilikuwa njiani na ilibidi itokee ili timu ibadilike kiuchezaji.
✍️ Eneo ambalo Simba SC ni dhaifu sana ni eneo lao la kujilinda. Hapa haina maana kuwa wachezaji wa eneo hilo sio wa daraja la juu bali jinsi timu inavozuia kama timu na si mchezaji mmoja mmoja.
✍️ Mimi sio mwalimu lakini tangu msimu huu umeanza golikipa wa Simba SC anafikiwa sana. Kuanzia kwenye mechi za ligi, Klabu bingwa mpaka AFL. kuna shida sana kwenye namna timu inavyozuia.
Hapa ilihitajika timu yenye ubora kumaliza nafasi zinazotengenezwa na Yanga wamefanya hivyo.
✍️ Ukuta wa Simba SC unafikiwa kiurahisi sana na kipa anafikiwa sana, yaani mara nyingi sana.. Hili ilibidi lije pengine kumkumbusha mwalimu kuset namna nzuri ya timu kuzuia. Hili lipo mikononi mwao
Msimu huu ni ngumu sana kuona Simba SC wamemaliza mechi bila kuruhusu goli kitu ambacho ni ishara mbaya kwao....
This was coming....
Nimefanya mahojiano na Shabiki wa Simba sc na shabiki huyu ameonekana kulia na kusikitishwa na kile kinachotokea katika mchezo wa leo .
0 Comments