Hot Posts

6/recent/ticker-posts

BARAKA MPENJA AIZODOA SIMBA KUPELEKEWA MOTO NA YANGA GOLI TANO AKA KONO LA NYANI🤣

Uploading: 354822 of 354822 bytes uploaded.


 NIMEWAHI KUSHUHUDIA MSIMU WA 2011/2012 Simba ikiichapa 5-0 YANGA katika mechi ya Ligi Kuu, Uwanja wa Benjamin Mkapa.


Nimewahi kushika MIC ya Azam TV nikitangaza SIMBA akiibamiza 4-1 YANGA KATIKA NUSU FAINALI YA ASFC, tena Wananchi wakipigiwa mpira mkubwa mno.


LAKINI NIMESHUHUDIA jana NOVEMBA 5, Wananchi Wakimpa HAMSA, Kono la Nyani Mnyama Simba, tena LUNYASI akiteseka kupita kiasi.


My God!, Yanga kwenye ubora mkubwa, walikuwa katili mno, Simba ilizidiwa kila eneo. Ilikuwa siku mbaya mno kazini kwa Wachezaji wa Simba. HAWATAHI kuitamani NOVEMBA 5, 2023.


Katika zama za Televisheni bora nchini Tanzania, Azam TV, MWANANCHI anaonesha kila kilicho bora uwanjani dhidi ya Mtani wake wa Jadi, Big up sana! Wananchi, poleni sana Simba. 


Huu ndio mpira, kuna nyakati mlifurahi na sasa mnahuzunika kama ambavyo Wananchi waliwahi kuhuzunika kwa nyakati tofauti.


Hii ndio haki ya MPIRA WA MIGUU. 


Hahahah! Karibuni kulima UMALILA. Mashamba nitawapa bure.

Post a Comment

0 Comments