Hot Posts

6/recent/ticker-posts

KILA MCHEZAJI ANAITAKA HII MECHI DHIDI YA SIMBA

 


Kiungo wa Yanga Maxi Nzengeli amesema hali ambayo inamshangaza kwenye timu yao ni kwamba kila mchezaji ananitaka nafasi ya kucheza mechi ya kesho dhidi ya Simba.


Nzengeli amesema "Hii ni mechi kubwa na hali niliyoiona hii wiki mazoezini imenipa uhakika wa hilo kutokana na maandalizi yetu,"alisema Nzengeli mwenye mabao matano katika ligi.


"Kumekuwa na hamasa kubwa baina yetu wachezaji kila mtu unamuona anapambana akiitaka hii mechi kwasisi ambao ni wageni imetupa hamasa kubwa ya kutaka ushindi.


Nzengeli ameongeza kuwa anaamini mbinu za makocha wao na ubora wa wachezaji wenzake utawafanya mashabiki wao kutoka na furaha kwenye mechi hiyo.



Post a Comment

0 Comments