Hot Posts

6/recent/ticker-posts

LIGI ITAISHA LEO KISAIKOLOJIA SIMBA VS YANGA




 KUELEKEA DERBY YA KARIAKOO

Simba inaingia kwenye mchezo wa watani wa jadi ikiwa imeshinda kwa 100% mechi zake sita tangu Ligi imeanza msimu huu. Kama Simba itaifunga Yanga ambayo ndio mpinzani wake namba moja kwenye Ligi itakuwa imeongeza tofauti ya alama na kuongeza kujiamini.


Yanga ikipata ushindi itakuwa imepunguza tofauti ya alama dhidi ya Simba katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu 2023|24.


Mechi za Simba na Yanga ni zaidi ya matokeo ndani ya dakika 90, ushindi huwa unatumika kujenga saikolojia. Timu inayoiwahi nyingine kutengeneza saikolojia nzuri mara nyingi huendelea kufanya vizuri. 


Simba imeuanza msimu vizuri japo ilikuwa haipewi nafasi wakati Ligi inaanza kutokana na ‘hype’ ambayo Yanga ilikuwanayo na ubora wa timu yao lakini Simba iliweza kucheza na kushinda kila mechi.

Post a Comment

0 Comments