Hot Posts

6/recent/ticker-posts

AZIZ KI MCHEZAJI BORA OCTOBER

 Kamati ya tuzo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemtangaza kiungo mshambuliajiw wa Yanga, Stephane Azizi Ki kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu kwa mwezi Oktoba akiwashinda Maxi Nzengeli wa Yanga na Moses Phiri wa Simba.



Azizi Ki ameifungia timu yake mabao manne katika dakika 278 za michezo mine aliyoichezea timu yake mwezi huu.


Kamati hiyo pia imemtangaza kocha wa Simba Roberto Oliveira 'Robertinho' kuwa kocha bora wa mwezi baada ya kushinda michezo yote mitatu aliyocheza mwezi Oktoba akiifunga Tanzania Prisons 1-3, Singida Big Stars mabao 1-2 na Ihefu 2-1.


Robertinho amewashinda Miguel Gamondi wa Yanga, abdulhamid Moalin wa KMC aliongia nao fainali 


Pia kamati imemtangaza meneja uwanja wa Higland estate mkoani Mbeya, Malule Omar kuwa meneja bora wa uwanja kwa mwezi Oktoba.

Post a Comment

0 Comments