Makocha wamesema, Robertinho anatakiwa kumuanzisha mshambuliaji Moses Phiri kama anataka matokeo chanya kikosini haswa kwenye dabi ya Jumapili.
Kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba, amesema “Mashabiki wanatakiwa kuelewa kuwa siyo wakati wote kocha atafanya wanachotaka hasa hawa wakigeni kikubwa ni Simba ina matokeo na sio Phiri kucheza kwani jambo la muhimu ni matokeo mazuri tu, ingawa kwa maoni yangu naamini akipata muda zaidi atafanya mambo makubwa.
Meja Abdul Mingange ambaye amewahi kuifundisha Mbeya City, amesema “Shida kubwa hapa Tanzania watu hatujui kuheshimu taaluma za watu, Robertinho yupo Simba kama kocha wa kigeni na anajua anaifundisha timu yenye presha ya aina gani hawezi kupuuza ubora wa mchezaji ambaye anaweza kumpa matokeo,”alisema Mingange.
“Kesi kama hii imewahi kutokea pale Chelsea wakati kocha akiwa Mourinho (Jose) na alipokuwa anatofautiana na mmiliki wa klabu kutaka Shevchenko (Andrea) apewe muda wa kutosha lakini kocha alisimama na msimamo wake hakuyumba.
Kocha Juma Pondamali aliyewahi kuitumikia timu ya Mashujaa, amesema; “Kumuingiza Phiri maana yake ni kwamba anataka kuusoma mchezo ili kupata matokeo mazuri na kuwadhuru wapinzani. Timu zilizoendelea huwa zikicheza ugenini haziwachezeshi wachezaji tegemeo ili wawasome wapinzani na wanapokuwa nyumbani wanawatumia ili kushambulia na kupata matokeo kwani hakuna mbinu mpya,”
0 Comments