Hot Posts

6/recent/ticker-posts

YANGA WANACHEZA KAMA VILABU VIKUBWA VYA ULAYA - OSAMA NABIH



Kocha wa klabu ya Al Merreikh, Osama Nabih amesema Yanga SC inacheza kama vilabu vikubwa vya Ulaya na kubainisha kuwa hatashangaa ikiwa Yanga itatwaa ubingwa wa Afrika.

“Tumekutana na vilabu vikubwa vya Afrika, lakini tulivyocheza dhidi ya Yanga, tumeona ubora wao wa kipekee.

“Sitashangaa ikiwa Yanga itatwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu. Wanacheza kama vilabu vikubwa vya Ulaya." amesema Osama Nabih.

Al Merreikh imeondoshwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia kipigo cha jumla cha 3-0 dhidi ya Yanga kwenye hatua ya pili ya mtoano.

 

Post a Comment

0 Comments