Kitu kingine kilichonipa furaha jana ni kuwaona mashabiki wa @yangasc wakipiga picha na kadi zao za Uwanachama pale Azam Complex ..👏
Yes, tumekwenda makundi ya Champions League baada ya miaka 25.
Na kama kuna siri kubwa nyuma yake basi ni vitu viwili tu
1: Uwezo wa kiuchumi wa Klabu yetu
2: Akili Kubwa ya viongozi 🧠
Vitu hivyo viwili ukivichanganya ndio unapata Quality Kubwa mnayoiona kwenye kiwanja leo.
Wakati huu tukisifia wachezaji wetu, Tukijivunia uwezo wa viongozi wetu .. Tusisahau kuiimarisha zaidi timu yetu kiuchumi.
Tunae GHALIB SAID MOHAMMED. Anafanya kazi kubwa sana kuhakikisha @yangasc Haiyumbi na kurudi ilipotoka.
Fedha anazotoa kuhakikisha Timu yetu inafika hapa ilipo leo hii ni nyingi mno.
Kama sio moyo wake wa ukarimu na mahaba yake na hii Klabu, pengine na sisi tungekuwa tunapokea vichambo kila siku.
Wanayanga Tumsaidie GSM sasa. Tuwasaidie viongozi wetu. Tuisaidie Klabu yetu.
Hii ndoto ya kuweka rekodi kubwa kwenye Ligi ya Mabingwa Msimu huu inaanzia kwetu kwa kulipia/kujisajili kuwa Wanachama halali wa Timu yetu.
Kama ulijisajili mwaka jana, muda wako wa mwaka mmoja umeshakwisha, Lipia tena Tsh 24,000 yako.
Kama bado, Usiwe mtu wa kuirudisha nyuma Klabu yako. Jisajili sasa kwenye Bank za CRDB/NMB kwa Tsh 29,000 upate na Kadi yako.
Kama tunavyotamani Furaha yetu iendelee, basi tuhamasishane na Usajili pia Uendelee
Sisi ni Klabu namba 3️⃣ kwa Ubora Afrika .. Tutafika kwenye kilele na kuwa namba 1️⃣ kama Tutashirikiana kwa pamoja kwa kila mtu kufanya jukumu lake
Viongozi wapange vizuri, Gamondi afundishe vizuri, Max atupe raha na sisi Mashabiki na Wanachama TUJISAJILI.
0 Comments