Hot Posts

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAKIRI SIMBA NA YANGA ZIMESAIDIA TANZANIA KUANDAA AFCON 2027


Serikali imetaja moja ya sababu iliyoipa nafasi Tanzania kuwa moja ya nchi itakayoandaa fainali za mataifa ya Africa (AFCON) kuwa ni Simba na Yanga.


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Damas Ndumbaro amesema idadi kubwa ya mashabiki wa Simba na Yanga na hamasa ndio kigezo moja wapo cha Tanzania kupata fursa ya ufunguzi au fainali ya Michuano Soka Barani Afrika (AFCON) 2027


Alitumia nafasi hiyo kuwataka mashabiki wa Simba na Yanga kuhamia kuziunga mkono timu za Taifa Ili kutoa hamasa ziweze kufanya vizuri.


“Hamasa ya mpira wa Yanga na Simba imekuwa chachu kubwa na ndio maana CAF wameweka mechi ya ufunguzi wa 'Super League' dhidi ya Al Hilal itakaofanyika Oktoba 20 mwaka huu jijini Dar Es Salaam," 


"Wajibu wa Serikali na Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tayari tumeleta Afcon Sasa kazi ipo kwa watanzania kuhakikisha wanaunga juhudi za wachezaji wa timu zote kupata sapoti,” amesema Waziri Ndumbaro.



 

Post a Comment

0 Comments