Hot Posts

6/recent/ticker-posts

YANGA NA UIMARA WA UKUTA WAO




✍️ Kuufungua ukuta wa Yanga SC imekuwa kazi ngumu na nzito sana kwa wapinzani wao msimu huu. Ni kazi ngumu kwelikweli kucheza dhidi ya Yanga na ukapata goli achilia mbali kushinda mchezo huo.

✍️ Eneo lao la ulinzi limezidi kuimarika siku baada ya siku. Tangu msimu huu uanze Wananchi wameruhusu goli moja tu kwenye wavu wao ndani ya dakika 90. Vuta picha, goli moja tu kwenye mechi takribani 9 za mashindani rasmi ambazo wamecheza mpaka sasa (tatu za ligi kuu, mbili za ngao ya jamii na nne za kufuzu klabu bingwa).

✍️ Ukuta chini ya Diarra, Metacha au Msheri, chini ya Ibrahim Bacca, Mwamnyeto na Job Dickson. Ukuta chini ya Yao Kouassi au Kibwana, Kibabage na Lomalisa. Goli moja tu ndilo ambalo ukuta huu umeruhusu mpaka sasa. Rekodi inatisha sana.

✍️ Muda mwingine siyo watu ulionao kikosini ila ni namna timu inavyocheza inakuwa ngumu sana kufikika kwenye eneo lao. Muda mwingi Yanga SC wanakuwa na umiliki wa mpira kwa asilimia kubwa hivyo watakuweka wewe busy kujilinda kuliko kuwashambulia wao.

Timu yenye ukuta bora nchini mpaka sasa ni Yanga Afrika.

GAMONDI anapika kwelikweli.....

 

Post a Comment

0 Comments