JKT TANZANIA V/s MASHUJAA FC ni mechi inayozikutanisha timu za taasisi zinazofanana [Jeshi la Kujenga Taifa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania] lakini pia ni mechi inayozikutanisha timu zilizopanda Ligi Kuu msimu huu, msimu uliopita zilikutana zikiwa Championship League.
Mashujaa FC wameanza vizuri Ligi, katika mechi nne zilizopita wameshinda mechi mbili na kutaka sare mbili, wana alama nne wapo nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi.
Wazee wa Mapigo na Mwendo [Mashujaa FC] hawajapoteza mechi [hawajadondosha alama tatu] na endapo leo watashinda basi wataongoza Ligi huku wakisubiri mechi ya Dodoma Jiji V/s Azam FC, kama Azam itashinda itawatoa nafasi ya kwanza!
JKT Tanzania ipo nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu baada ya kucheza mechi nne, imeshinda mechi moja, imetoka sare mechi moja na kupoteza mechi mbili, hivyo ina alama nne.
Matokeo ya ushindi leo yataifanya JKT Tanzania kufikisha alama saba sawa na KMC FC na kupanda hadi nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi.
0 Comments