Hot Posts

6/recent/ticker-posts

JERRY MURO AANDIKA MAKUBWA KWA YANGA BAADA YA KUFUZU KLABU BINGWA


Historia ni mwalimu mzuri sana, tunaitunza hii historia tukufu kwa ajili ya vizazi vyetu vijue tuliendelea walipoishia wenzetu baada ya zaidi ya miaka 20 na sasa tunaendelea mbele zaidi tukiwa wamoja na imara zaidi.

Mungu awatangulie wananchi @yangasc katika maandalizi ya safari ya hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa barabi Africa @caf.championsleague, tunaimani na uongozi @caamil_88 pamoja na bench la ufundi na wachezaji kuwa safari hii tutasonga mbele zaidi

Mungu aendelee kukubariki Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia katika kuongoza hamasa na kuwezesha sekta ya michezo nchini na haya ni matunda yanaendelea kuonekana na ni fahari yetu sote, tunaamini michezo ni moja kati ya matukio yanayotuleta pamoja watanzania wote bila kujadili dini, itikadi za siasa na makabila katika michezo sote tunazidi kuwa wamoja Daima.

#TeamWananchi #MichezoYetu #SSH

 

Post a Comment

0 Comments