Hot Posts

6/recent/ticker-posts

UNAMJUA JAY JAY OKOCHA WA NIGERIA NA PSG ENZI HIZO WEWE? HII NDO STORY YAKE KIDOGO


Akiwa nchini Tanzania kukuza mashindano ya Kombe la Dunia la Wachezaji wa Zamani mwaka 2024 (VCWC), nyota wa zamani wa soka duniani, Augustine Azuka Okocha maarufu Jay-Jay Okocha, ambaye aliyejipatia umaarufu katika Ligi Kuu ya England na Kombe la Dunia la FIFA amesema kuwa afya ya akili ni muhimu kwa kila binadamu, si tu wanamichezo.

"Mara nyingine watu wanasahau kuwa sisi (wanamichezo) pia ni binadamu, na inaweza kuwa ngumu kusimamia umaarufu na matarajio. Siwezi kusema mengi kuhusu wakongwe wote kwa sababu sipo nao wote. Wale ambao nipo nao tunashirikiana kwa mawazo na kujaribu kuendelea kuwa karibu. Nadhani ni muhimu kuweza kujishughulisha. Hilo, kwangu mimi, ndilo linaweza kusaidia mtu kushughulikia afya ya akili," amesema Okocha.

Pia amezungumzia umuhimu wa kuwa na mpango wa pili katika maisha. 
"Soka hutoa msingi wa kujengea, ni kazi fupi sana. Wengi wa wanamichezo wanafanya vizuri leo ikilinganishwa na wakati wetu kwasababu kuna ufahamu zaidi, tofauti na wakati wetu ambapo kila kitu kilikuwa cha analogi.

Okocha anatajwa kama mmoja wa wachezaji bora wa soka kutoka Afrika. Alicheza kama kiungo mshambuliaji, akiichezea taifa ya Nigeria kati ya mwaka 1993 na 2006, akifunga mabao 14, na alikuwa mwanachama wa timu tatu za Kombe la Dunia la FIFA.

Ulaya, Okocha aliichezea PSG, Frankfurt, na Fenerbahce na akajipatia umaarufu katika Ligi Kuu ya England akiwa Bolton Wanderers na Hull City.

Via mwanaspoti

 

Post a Comment

0 Comments