Hot Posts

6/recent/ticker-posts

TAIFA STARS RASMI LEO KUJIJUA WAKO UPANDE GANI


TIMU ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars, 🇹🇿 leo itafahamu wapinzani wake watatu katika kundi kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 zitakazofanyika mwakani huko Ivory Coast 🇨🇮 baada ya droo itakayochezeshwa Abidjan, nchini humo kuanzia saa 3 usiku.
.
Kwenye droo hiyo itakayoongozwa na kusimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Tanzania itakuwa katika chungu cha nne pamoja na Guinea Bissau, Msumbiji, Namibia, Angola na Gambia.Kwa mujibu wa utaratibu uliotolewa na CAF uchezeshaji wa droo hiyo kutakuwa na makundi sita yatakayoundwa na timu nne, moja kutoka kila chungu kati ya vinne vitakavyokuwa na timu sita kila kimoja kulingana na nafasi ambayo ipo katika viwango vya ubora.
.
Timu mwenyeji, Ivory Coat itapangwa kundi A na hivyo inasubiri nyingine tatu kutoka katika chungu namba mbili, tatu na nne. Kitendo cha Tanzania kuwekwa katika chungu cha nne kinaiweka katika uwezekano wa kupangwa kundi gumu kutokana na ubora wa vikosi na wachezaji wa timu zilizopo katika vyungu vitatu tofauti na ambacho Taifa Stars ipo.



 

Post a Comment

0 Comments