Ndani ya Brighton yupo bwana mdogo mmoja wa kuitwa CARLOS BALEBA. Huyu ni raia wa Cameroon ambaye amejiunga na klabu hiyo kwenye dirisha lililopita akitokea Lille ya Ufaransa.
Alikichafua sana kiungo cha Brighton kwenye sare yao ya 2-2 dhidi ya Liverpool weekend iliyopita. Alipora sana mipira pale katikati, aliituliza timu kisawasawa na akaamua icheze kwenye tempo anayoitaka yeye. Bwana mdogo tu wa miaka 19 tena mwenzetu kabisa yaani ngozi na roho ya Kiafrika.
Kumbuka eneo analocheza yupo pia Bill Gilmour na Dahood ambao kila wakipewa nafasi wanafanya balaa lakini Baleba aliaminiwa kwenye mechi dhidi ya Liverpool na ni mechi ya ligi kuu na akakichafua dakika zote 90.
Mimi sio mtabiri lakini nina amini kuwa hili ni jina lotakalosumbua sana kwenye madirisha ya usajili muda sio mrefu...
Carlos Baleba 🔥
0 Comments