Hot Posts

6/recent/ticker-posts

UKOSOAJI WETU USIFUNIKE PONGEZI KWA SIMBA SC...



✍️ Wengi wetu tunaikosoa sana Simba SC na kudai kuwa haturidhishwi na namna timu hiyo inavyocheza. Hatujaridhika na jinsi timu hiyo ilivyocheza mechi yake dhidi ya Power Dynamos. 
Ni kweli tuna haki hiyo ya kukosoa na kuuongelea upande mbaya wa timu hii.

✍️ Lakini ukosoaji huu umefunika ubora mkubwa sana wa Simba SC. Wengi tunasahau kuwa siyo kila mwaka timu itatinga hatua kama hizi kibabe. Timu zinajipanga sana zikiona mbele yao kuna Simba SC, makocha wanafanya home work ya kutosha na wachezaji wa timu pinzani wanajua hii kwao ni zaidi ya mechi ya kawaida kwani mpinzani ni mgumu sana.

✍️ Siku zote tusipende kumuongelea fulani kwa kumlinganisha na mwingine. Ni kweli Simba SC inabidi waboreshe uchezaji wao lakini hii isitunyime fursa ya kuwapongeza kwa kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa kwa mara ya sita. Mara sita ni nyingi sana.

✍️ Football ni mchezo wa wazi ndiyo maana kila mtu atasifia na mwingine atakosoa kutokana na kile alichokiona yeye.
Lakini kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika mara sita kwa klabu kutoka ukanda huu ni kubwa sana.

Ukosoaji huu usifunike pongezi zetu kwa klabu hii...

✍️mlelwa_fred

 

Post a Comment

0 Comments