✍🏻Chelsea ilikuwa timu bora zaidi uwanjani kwa muda mrefu sana na hata ukiangalia kwa nafasi zilizotengenezwa pengine Chelsea wangeshinda magoli mengi zaidi ya haya .
✍🏻Kipindi cha kwanza vitu viwili viliwatafuna Fulham
1: Pereira na Reed walikuwa wanachelewa kuwafanyia pressing Enzo na Caicedo na ukizingatia ufundi wa viungo hao wawili wa Chelsea : one touch football ilikuwa inatosha kuwafanya waitoe timu nyuma na kufika mbele haraka
2: Position ya Gallagher pale Chelsea hawana mpira , alikuwa anafanya man marking dhidi ya Palhinha wakati Palmer alikuwa ana bend pressing yake dhidi ya Tim Ream ... faida yake ? Inawalazimisha Fulham kufanya haya :-
A: Kupiga mipira mirefu ambayo Chelsea walikuwa wanaishinda
B: Kuwalazimisha Fulham kwa kufanya makosa ( kulazimisha kucheza kuanzia chini ) na ndio goli la pili lilipotokea
✍🏻Kipindi cha pili baada ya Fulham kufanya mabadiliko kuingia kwa Iwobi na Vinicius angalau kidogo walionekana wanacheza na kutengeneza nafasi yao bora kwa Lukic ... walichotumia zaidi ?
::: Ni switching play kwa Castagne mipira mingi sana ilikuwa inafika kwake lakini krosi zake hazikuwa zinashambuliwa na wachezaji wengi
NOTE
1: Cole Palmer : passing , kutunza mali , touches zake , utulivu wake akiwa pressed . Na pia Pochettino kapatia sana jinsi ya kumtumia , sio ile winger kabisa bali anaingia ndani kwenye halfspaces nyuma ya mstari wa kiungo wa Fulham
2: Enzo na Caicedo one touch football yao iliwasumbua sana Fulham hasa kipindi cha kwanza
3: Pasi ya Colwill 🔥 Control na finishing ya Mudryk
4: Raul Jimenez kaenda mechi 30 bila kufunga goli ( Wolves na Fulham ) 🤔🤔
5: Conor Gallagher energy yake uwanjani ni muhimu sana kwa Chelsea
6: WALIKUWA WANASUBURI MDHAMINI MPYA KUANZA LIGI RASMI : THE BLUES HAO
FT: Fulham 0-2 Chelsea
0 Comments