Utakuwa unafanya makosa ukiwa unamuongelea Roberto Oliveira huku ukikitazama kikosi cha Yanga SC na kuanza kufananisha uwezo wao
Ndio nawaelewa mashabiki wa Simba kuhusu muendelezo wa kikosi chao, huku nitawaelewa zaidi wale wote wanaokoa uwezo wa Kocha huyu huku wakisema hawaelewi nini plan yake
Wana Lunyasi hawajazoea kucheza nyumbani halafu waondoke vichwa chini hayo siyo mazoea yao hata kidogo
Timu inashinda mashabiki wanashikilia moyo dakika zote za mchezo, hakuna ile raha kwao huku ikiwa tofauti na Watani zao Yanga ambao wao dakika nyingi ni shangwe zaidi
Hata hivyo naamini benchi la Simba SC chini ya Kocha Mkuu Robertinho Oliviera atakuwa ameliona hilo na atalifanyia kazi kwa haraka, watu wa Simba siyo wavumilivu hua hawezi kutilia pale wanapoiona timu yake haichezi lile soka la Samba, soka safi lenye minyama nyama kwenye pitch
Hongereni wana Simba SC Kubwa timu imefuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika
Hapa ni kuanza maandalizi ya kujiweka fiti kwani Octoba 20, 2023 kikosi cha Simba SC kinaenda kukabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Mafarao Al Ahly katika michuano mipya ya Super Cup Afrika.
0 Comments