Hot Posts

6/recent/ticker-posts

WACHEZAJI WA SIMBA WALIONEKANA TIMU YA TAIFA HADI SASA NI HAWA


Wachezaji wa Simba Kibu Denis na Mzamiru Yassin wameonakena kwenye mazoezi ya kikosi cha timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars' kinachojiandaa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Sudan.


Mechi hiyo itapigwa Oktoba 18 nchini Saudi Arabia na mastaa tayari washaingia kambini kujiandaa na mechi hiyo.


Wakati mechi hiyo ikipigwa Oktoba 18 itakuwa bado siku mbili Simba SC kucheza mechi ya ufunguzi ya African Football League dhidi ya Al Ahly katika uwanja wa Mkapa jijini Dar (Oktoba 20) huku wapinzani wao Al Ahly tayari washatoa taarifa ya kuwazuia mastaa wake wakiwemo Percy Tau kujiunga kikosini Afrika Kusini na Aliou Dieng kwenda Mali.


 

Post a Comment

0 Comments