Supastaa wa Inter Miami, Lionel Messi ameteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Marekani (MLS) licha ya kucheza mechi nne tu.
.
Bingwa huyo wa Kombe la Dunia alijiunga na Inter Miami na kuingia moja kwa moja katika timu akiwaisaidia kubeba ubingwa wa Kombe la Ligi kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo, huku akifunga mabao 10. Lakini, licha ya kuwa na takwimu nzuri baada ya kucheza mechi chache, mashabiki wameshangaa sababu ya Messi kujumuishwa katika orodha ya majina wanaowania tuzo ya mchezaji bora katika ligi hiyo.
.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 alicheza michezo minne ya msimu wa kawaida katika klabu hiyo inayomilikiwa na David Beckham kabla ya kusumbuliwa na majeraha. Katika michezo hiyo, amefunga mara moja na kutoa asisti mbili za mabao lakini bado mashabiki wamedai hakustahili kuwemo katika orodha hiyo.
.
Licha ya takwimu zake kutoridhisha Messi ameteuliwa kuwania tuzo ya MVP wa Ligi Kuu Marekani ambayo imepewa jina la gwiji wa zamani wa timu ya taifa ya Marekani, Landon Donov.
0 Comments