.
“Sikiliza, ni kweli naiona hiyo hali, mashabiki waje uwanjani kuangalia Simba inacheza mpira vizuri. Kwangu Bocco bado ni mshambuliaji mzuri kwani anakwenda kufanya kile ninachokitaka afanye,” alisema Robertinho na kuongeza;
.
“Hata katika mechi dhidi ya Dynamos (Power) aliingia akafanya nilichotaka tukapata bao lililosaidia kutuvusha makundi na leo (juzi) nimempa nafasi ya kuanza amefunga tena, lakini akawafanya mabeki wa Prisons kwa muda mwingi kubaki nyuma, nataka mshambuliaji wa aina hii anayekaa muda mrefu eneo la hatari la wapinzani na hili ndicho anafanya Bocco huyu bado ni bora kwangu.”
.
Kocha huyo alisema anao washambuliaji wengine kama Jean Baleke na Moses Phiri ambao nao ni wazuri kwa kukimbia pembeni lakini wamekuwa hawajaweza kucheza kwa nidhamu kama anavyofanya Bocco.
.
“Simba tunajivunia kuwa na washambuliaji wengi wazuri, kwa Baleke na Phiri angalieni tu, muda mwingi wanataka kukimbia pembeni hili linatufanya kushindwa kutumia vizuri nafasi tunazotengeneza tunaendelea kuwaongezea ubora huo na wao ili wacheze kama Bocco.
.
“Nimezungumza na Bocco nimemwambia aachane na mambo ya mashabiki anisikilize mimi kama kocha wake, mashabiki wanataka ushindi hesabu zetu ndio zitakazowapa furaha, unaona amefunga wamenyamaza nataka aendelee kufanya hivyo hivyo kila mara kwani nitaendelea kumtumia,” alisisitiza Robertinho aliyefikisha jumla ya mechi 15 bila kupoteza katika Ligi Kuu.
0 Comments