KUNDI D hili linajumuisha timu zote ambazo ni mabingwa kwenye mataifa yao [Al Ahly, CR Belouizdad, Yanga na Medeama].
Al Ahly ni mabingwa wa Misri msimu uliopita lakini pia ni bingwa mtetezi wa Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika ambalo alichukua msimu uliopita baada ya kuifunga Wydad Athletic.
CR Belouizdad ni mabingwa wa Algeria mara nne mfululizo, ambao kwa sasa Kocha wao Mkuu ni Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa zamani wa Simba.
Yanga ni mabingwa wa Tanzania mara mbili mfululizo kwa misimu miwili iliyopita tena wakiwa wamecheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita!
Medeama wenyewe ni mabingwa wa Ghana msimu uliopita, timu hii ambayo imeanzishwa mwaka 2002 imeanza kusumbua kwenye soka la Afrika.
0 Comments