Wanachama wa Mkutano Mkuu wa TEFA wakafanya Mkutano wa kikatiba na kuridhia kwamba, Makamu Mwenyekiti wa kwanza akaimu nafasi ya Mwenyekiti aliyefariki na Makamu wa pili akaimu nafasi ya Makamu wa kwanza halafu wasubiri uchaguzi mkuu mwezi Machi mwakani.
Wakampitisha Makamu Mwenyekiti wa kwanza akainu nafasi ya Mwenyekiti aliyefariki mpaka Mkutano Mkuu wa uchaguzi watakapofanya uchaguzi kujaza nafasi hiyo kwa mujibu wa taratibu na kanuni za katiba yao.
Yakaja maelekezo ya kutengua maamuzi ya kikatiba yaliyofanywa na TEFA, kwamba uchaguzi uitishwe tena nao kwa kutii wakafanya.
Watu wakachukua fomu, miongoni mwao akiwa ni Makamu wa kwanza na Makamu wa pili na wajumbe wengine. Wakafanya usaili yakapita majina yote
Baada ya hapo likatolewa agizo na DRFA Kamati ya Uchaguzi ya TEFA haina sifa ya kusimamia ule uchaguzi mchakato uhamie DRFA.
Baada ya mchakato wa uchaguzi kuhamia DRFA, usaili ukafanyika upya na hapo ndipo ‘wakachinja’ wagombea wote na kubakiza jina la mtu mmoja!
Mtu aliyebakizwa hajawahi hata kuwa kiongozi, hajawahi kuwa hata mjumbe wa kamati! Mtu huyu ndio anaonekana ana sifa kumshinda Makamu wa kwanza na wapili wa TEFA ambao wameonekana hawana sifa.
0 Comments