Hot Posts

6/recent/ticker-posts

TIAFA STARS NI AMA ISONGE MBELE AMA ISHIKE MKIA KUNDI LA NGUMU KUMEZA AFCON


Mchezaji wa zamani wa Taifa Stars @amrikiembatz anatamani kuona Tanzania ikipangwa kundi moja na Ivory Coast [wenyeji wa mashindano], DR Congo na South Africa.

KUNDI KIEMBA

🇨🇮 Ivory Coast
🇨🇩 DR Congo
🇿🇦 South Africa
🇹🇿 Tanzania

Kiemba amesema hapo bafasi moja ya kufuzu hatua ya 16 bora tayari unampa mwenyeji [Ivory Coast] halafu inabaki nafasi moja ambayo tutaipigania Tanzania, DR Congo na South Africa.

“Hivi karibuni kwenye madaraja hatupishani sana na DR Congo lakini bado wanaonekana wapo juu yetu, lakini mwingiliano wa wachezaji DR Congo na aina yao ya uchezaji unaweza kutusaidia na sisi kujua wapi tunaanzia.”

“South Africa wale ni wenzetu kama timu ya Taifa ya England, hawana mwendelezo mzuri kwa hiyo unaweza kuwakuta kwenye michuano wapo unga kuliko hata sisi.”

“Kwamaoni yangu nadhani kundi hilo kama tunajipanga vizuri tunapata nafasi miongoni mwa timu mbili zinazoweza kufuzu hatua inayofata.”

 

Post a Comment

0 Comments