Ni Simba SC inarudi kilele cha msimamo wa Ligi Kuu NBC PL, 2023/2024
Ni alama 12 ikijikita huku Yanga SC ikisimama na zake alama 9 yes ni kibabe zaidi
Kuhusu kiwango siwezi kusifia sana lakini kiuchezaji inacheza kimkakati halafu matokeo yanapatikana, nguvu inatoka wapi?
Kelele za mashabiki na maneno makali pengine zinawaingia Wachezaji (siungi mkono aina ya ushabiki huo), Kisha viongozi wanawaletea hizo clip na kuwakumbusha kuhusu hilo na kuwaambia, mna deni juu ya hawa watu
Kushinda Sokoine, MBEYA siyo rahisi hata kidogo, uwanja mgumu ule lakini Simba SC 'Mnyama' anaondoka na alama tatu na Mabao matatu kibindoni
Mitaa yote inaongea, Mnyama Kashinda Mwananchi kaanguka, mashabiki wanatambiana huku kuzodoana kukichukua nafasi Kubwa
Hata hivyo ningependa kuwakumbusha watu hapa, msiishi kwa kukariri msije mkasema eti mbona iliwahi kuwa hivi na itakuja kuwa vile tena, tusikariri kila siku
Viongozi wa Simba SC walikaa na walijua wapi walipoangukia, haitakuwa rahisi kuacha lile la msimu mwaka jana litokee, hawatakuwa tayari habadani.
Niulize, je bado wapo wale wanaotaka kocha Robertinho Oliviera aondokee?
0 Comments