Hot Posts

6/recent/ticker-posts

MCHEZAJI WA BARCELONA ALIVYOPONZWA NA CHOO SIKU YA MECHI YA UEFA VS PORTO


 KINDA wa Barcelona, Lamine Yamal alisherehekea ushindi wa kihistoria kwa upande wake dhidi ya Porto katika mechi ya Ligi Mabingwa Ulaya Jumatano usiku, lakini alilamizika kutoka nje ili kwenda chooni.

.

Kinda huyo alianzishwa kwa mara ya kwanza katika mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Porto wakiibuka na ushindi wa bao 1-0. Akiwa na umri wa miaka 16 na siku 83, kinda huyo amekuwa mchezaji wa kwanza mdogo zaidi kuanza katika michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya.

.

Wakati Barcelona inaongoza kwa bao 1-0 lililowekwa kiamini na Ferran Torres kinda huyo alitumia mwanya huo akaenda chooni. Ilipofika dakika ya 71 ya mtanange huo kinda huyo alilazimika kutoka uwanjani kwenda chooni kwa mara nyingine wakati mechi inaendelea. Lakini Yamal hakurejea kuendelea na mechi kwani kocha Xavi Hernandez alimfanyia mabadiliko dakika ya 80 huku Barcelona ikicheza ikiwa pungufu dakika 10 kabla ya mechi kumalizika.



Post a Comment

0 Comments