Hot Posts

6/recent/ticker-posts

"KAMA MKONO WA MARADONA...KAMA MGUU WA EMI MARTINEZ"



Yapo matukio mengi sana ambayo yanamtokea mtu na anayasahau. Yapo yale ambayo hata itumike nguvu kubwa kumkumbusha bado hatakumbuka. Lakini yapo matukio ambayo haihitaji hata kukunbushwa, mtu unayakumbuka tu mwenyewe.

Kama ambavyo wapenzi wa soka nchini Argentina hawahitaji kukumbushwa kuhusu lile bao la mkono la Diego Maradona, ndivyo ambavyo hawahitaji kukumbushwa kuhusu ile save ya mguu wa kushoto wa EMILIANO MARTINEZ. Hata bila kukumbushwa, wanaakumbuka tu wenyewe.

Tayari Waargentina walishashika vichwa kukata tamaa, Wafaransa walishainuka majukwaani tayari kuimba jina la Randal Kolo Muani. Lakini haikuwa hivyo kwa Emiliano Martinez, mguu wake wa kushoto ukatandazwa kuzuia kilio ambacho kingeikumba Argentina.

Mbali na mikwaju mingi ya penati aliyoichomoa Emi, hili ni tukio ambalo wengi wanalikumbuka sana na bila shaka hata yeye atakuwa analikumbuka sana tukio hilo.

Kama mkono wa Diego Maradona.... Kama mguu wa kushoto wa EMILIANO MARTINEZ....

✍️ mlelwa_fred

 

Post a Comment

0 Comments