Binafsi nawahusudu sana makocha wenye akili nyingi sana linapokuja suala la kutengeneza timu ya ushindani kwa kuzingatia mbinu kulingana na mechi.
Jose Mourinho moja ya makocha bora kabisa kwenye football kwasababu ya namna ambayo anaweza kucheza mechi kulingana na mpinzani.
Jose akikutana na timu yenye uwezo wa kumiliki mpira kuliko yeye mara nyingi uchagua kuwa timu ya pili kiwanjani,uchagua timu yake kukaba na kukimbia kilomita nyingi,Jose akikutana na timu ambayo hana haja ya kupaki basi anacheza kwa kufunguka tu.
Ukienda kwa Pep Guordiola naye aina Kocha ambaye anajua sana mbinu za mpira wa miguu kwasababu ana maarifa ya kutosha,Pep mara nyingi anapenda kucheza mechi na kutumia wachezaji kwenye mbinu tofauti kumbuka jinsi ambayo aliamu kumtumia John Stone kwenye midfield wakati John Stone ni beki.
Mara nyingi makocha ambao wamefika wenye daraja la juu ( Intellectual Elite Coaches) wanakuwa na Sifa hizi
📌1.Kutumia wachezaji kulingana na mechi huiska
📌2.Kucheza kwa muundo toufauti kulinga na mpinzani.
📌3.Kubadilika kulingana na mazingira ya mchezo.
Kocha Robertinho Akicheza na Ihefu ni tofauti sana akicheza na Al Ahly,ni aina mwalimu ambaye level yake tactics ni kubwa sana kwasababu ana maarifa sahihi ya kusoma mazingira ya mpinzani.
Robertihno hawezi kuwa Pep hawezi Mourinho lakini anafanya vitu sawa na hawa watu.
@omarrkombo
0 Comments