Hot Posts

6/recent/ticker-posts

JONAS MKUDE AJIPANGE UPYA YANGA BADO ANAO MUDA WA KUFANYA MAKUBWA JANGWANI NA KULIPA HESHIMA

 


Kiungo Jonas Mkude ana deni na Yanga na muda wa kuilipa anao, anachotakiwa ni kukaa chini na kutafakari aanzie wapi dhidi ya anaoshindania nao namba ndani ya kikosi hicho, kisha achukue hatua.


Gamondi aliwahi kusema kwamba; ”Kila mchezaji ana nafasi ya kucheza ndani ya kikosi changu, ninachoangalia ni bidii yao mazoezini, kwani lengo ni timu kufanikiwa kwenye malengo yake.”


Beki wa zamani wa Simba na Yanga, Amir Maftah alisema bado anaamini Mkude ana uwezo wa kucheza kikosi cha kwanza kwa sharti ya kumuonyesha kocha anachokitaka akifanye.


“Kocha anapompa mchezaji dakika za kucheza anakuwa na maana kubwa ya kuangalia je, anakifanya kile anachotakiwa, ndio maana nasema Mkude ni yeye kujipanga ila bado ana umri wa kucheza na akabadili upepo,”alisema.


Hoja yake iliungwa mkono na staa wa zamani wa Simba na Stars, Steven Mapunda aliyewatolea mifano Clatous Chama na Moses Phiri kwamba mashabiki waliwatetea mbele ya kocha wao Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ilitokana na uwezo wao.


“Ninachokiona kwa Mkude anapaswa kujipanga na kujitoa kweli kweli kurejesha kiwango chake ni kiungo mzuri sana akikaa kwenye mstari. Ukiona mashabiki wamenyamaza na hawamwambii kocha akupange jiulize mara mbili mbili na lazima ukubali ukweli ambao utakubadilisha,” alisema.

Post a Comment

0 Comments