Hot Posts

6/recent/ticker-posts

SIMBA NA YANGA SAFARI SIO NDEFU ZITABEBA KOMBE LA AFRIKA

 


Nimewatazama jana Al Ahly tena dhidi ya Mamelodi Sundowns kisha baadae nikawatazama Esperance na Wydad, nimezitazama mechi zote vyema sana nimeshawishika kusema MO na GSM hawana safari ndefu sana ya kufika walipo ila WAKUNJUE HASWA POCHI zao, ndio namna pekee ya kufika walipo Jamaa. 

Sasa hivi ndio sehemu pekee iliyobaki nayo ni PESA ama UKWASI, Makocha kwasasa wanakuja nchini tena wazuri tu shida ni QUALITY flani tunaikosa kubwa ya Wachezaji, Mamelodi na Mazembe kutoka Kusini huku mwa Jangwa walibeba ndoo kwakuwa wana huo Uwekezaji mkubwa nje na hapo ni stori. 

Kama Simba iliweza kumpa mechi nzito sana Al Ahly ikiwa tangu Julai, 2023 ndio mara ya mwisho kuruhusu chuma mbili langoni mwake tena dhidi ya Pyramids halafu anakuja kuruhusu mbele ya Simba, mechi mbili zote zimelala pacha sio kitu rahisi. 

MATAJIRI wa Kariakoo kilichosalia sasa ndio hizo sajili za BILLION zinazotajwa, Wenzetu wanaenda Ulaya wanavunja mkataba wanaleta mali Afrika, wale Mamelodi wana mtoto kutoka Chile ambaye alienda mpaka Arsenal ana thamani ya BILLION SITA walinunua, hizo ndio levels sasa! 

Kwasasa MATAJIRI ndio mmesalia kutuvusha hapa tulipo. 



Post a Comment

0 Comments