Mashujaa FC, Tabora United na JKT Tanzania ni timu tatu [3] ambazo zimepanda Ligi Kuu msimu huu 2023|24, timu hizi zimefanikiwa kukaa katika nafasi saba [7] za juu baada ya mechi tano [5] Ligi.
Mashujaa FC na Tabora United zote zina alama nane [8] baada ya kushinda michezo miwili, sare mbili na kupoteza michezo miwili. Mashujaa FC ipo nafasi ya tano [5] huju Tabora United ikiwa nafasi ya sita [6].
JKT Tanzania ipo nafasi ya saba [7] ikiwa na alama saba [7] baada ya kushinda michezo miwili, sare moja na kupoteza michezo miwili.
Ukiangalia timu kama Tabora United ilivyoanza mechi yake ya kwanza ya Ligi dhidi ya Azam FC halafu sasa hivi ipo pale nafasi ya tano [5] si jambo la kubeza! Inaonesha wamekuja Ligi Kuu kushindana sio kushiriki.
0 Comments