AHMED ALLY, kama kuna kitu ambacho kiliacha maswali mengi ni nani atavaa viatu vya Haji Manara ndani ya Simba mtihani mgumu sana ambao ulihitaji utulivu mkubwa sana, binafsi yangu huwa nakiri ni miongoni mwa maamuzi bora ya mwisho mwisho kwa CEO @bvrbvra kabla hajaondoka ndani ya Simba basi ni kumleta Ahmed ndani ya Simba.
Unajaribu kuwaza ugumu wa kazi ambao aliingia na kukutana nao? Timu haina makombe huu ni msimu wa tatu sasa umeanza, lakini kama Meneja wa Habari anaifanyaje Simba kuwa relevant mtandaoni? Lazima awe Afisa na bado awe ni propaganda tool kitu ambacho amekipambania na kukiweza kwa asilimia kubwa, maua anapaswa kupewa.
Sote tunafahamu uwezo mkubwa na idadi ya Wafuasi wa wenzake lakini yeye alipoingia akairudisha kwanza timu kwa watu mtaani, aliitoa timu Masaki na kuipeleka Buza, Sinza, Yombo, Ubungo na kila sehemu, Mjanja Mjanja alitaka ngoma ichezwe na Mashabiki wote, hapo ilikuwa akili ya kwanza kubwa ya kupandisha maji mlima.
Ahmed kwasasa anakosa vitu viwili tu ambavyo sio kazi yake, ni kazi ya wengine kwenye mfumo wa utawala! Anakosa makombe ya kuendelea kumpa nguvu, anakosa vifaa (uwekezaji) wa maana kwenye Idara yake, tukiri wazi kuwa kwenye suala la vifaa tupo nyuma sana na hilo sio kosa lake, ni suala la kiofisi na uwekezaji wao.
Ni wakati wa kurejesha tena namba ambazo zimepotea kwa kiasi kikubwa! Maboss wawekeze kweli, teknolojia nzuri kuanzia camera za kueleweka, vifaa vya maana kuendana na timu kubwa, ni aibu mara Youtube sauti hakuna, mara matangazo kama masela, ni lazima uwekezaji ufanyike ili vita ya namba mtandaoni irejee, maudhui ni pesa, lakini lazima utoe pesa.
My Brother Chinga @ahmedally_ ameamua kuvivaa viatu kwa style yake hata pale timu ipo kwenye presha amekuwa mtulivu, amekuwa nuru kwenye giza na Mashabiki huwa wanamheshimu kwenye hilo, binafsi navutiwa sana na kazi yake pamoja na Idara yake nzima, they are doing a great job kwenye maeneo yao na juhudi zinaonekana.
Kinachosalia ni CEO wa sasa kukunjua mfuko Vijana wapeleke mahitaji yao mezani! Idara yao imetimia wala haina shida, Mungu awabariki sana.
0 Comments