Hot Posts

6/recent/ticker-posts

Ooooh HIVI KUMBE?


Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Iman Kajula akizungumza leo na waandishi wa habari amesema Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Ptrice Motsepe atakuwepo na marais wa vyama vya soka maeneo mengine akiwemo Rias wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Gianni Infantino katika mechi ya uzinduzi wa 'African Football League' Simba dhidi Al Ahly Oktoba 20.

"Rais wa FIFA atakuwepo, Rais wa CAF atakuwepo na marais wa vyama vya soka vya maeneo mengine hivyo inahusisha vyombo vingi za serikali." amesema Kajula

Kajula amezungumzia ukarabati wa Uwanja wa Mkapa na ameishukuru Serikali kwa ukarabati huo ambapo kufika Oktoba 9, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Damas Ndumbaro alisema ukarabati umefika asilimia 95 

"Tunaishukuru serikali kwa matengezo makubwa ambayo imefanya kwenye Uwanja wa Mkapa. Simba pia imetoa mchango kiasi kufanikisha hili."

 

Post a Comment

0 Comments